WATENDE KIYAGI

Mtoto wa Mitaani
‘Sikuweza kumaliza shule kwa sababu ya ukata ulioikabili familia. Kila nilipopelekwa shuleni, nilitoroka. Nilitorokea visiwani, machimboni na, hata, mijini nikitafuta namna ya kuikwamua familia ili tuondokane na umasikini. Kupitia kutafuta huku, hatimaye, Maisha yangu yakawa ya mitaani. Nilidharaulika, jamii ilinitelekeza na kuonekana kama mtoto asiyefaa. Lakini Mungu, kwa wingi wa rehema, amenufanikisha. Ninamiliki kampuni, nyumba, na magari kadhaa hapa hapa Dar es Salaam.’

Endelea Kusoma Sikiliza Tazama

BAYOMBYA MADULU NDAKI

“Tamaa ya maisha, uporaji na ujambazi, yalipelekea nipigwe risasi, tumbo likafumuka, utumbo wote ukamwagika nje, lakini kwa rehema za Mungu, nikapona. Wenzangu wanne niliohukumiwa pamoja nao, walifia gerezani, mimi peke yangu, nimeokoka na sasa niko huru kuhubiri habari njema. Mungu alinitendea mambo makuu ambayo sitaacha kuyasimulia.”

Endelea Kusoma Sikiliza Tazama

CHARLES LUOGA

Mimi nimekuwa shahidi wa matendo makuu ya Mungu. Nimelisoma na kuliishi neno lake. Nimemuona Mungu akinitendea na kuwatendea wengine.Pia, nimewaona watu mbali mbali, katika huduma yangu na kwingineko, wakiendelea kuukulia wokovu. Kupitia muujiza huu, pendo na utumishi wangu kwa Mungu vimeongezeka. Ninataka nikuhakikishie wewe, unayeusoma ushuhuda huu, kuwa Mungu yupo. Anatenda miujiza, huwalinda watu wake, na kuwaponya

Endelea Kusoma Sikiliza Tazama

COSMAS CHIDUMULE

Maisha ya starehe nyingi, nilipokuwa katika ulimwengu wa muziki duniani hayakunifanya nifikie kwenye utoshelevu wa furaha na amani ya kweli moyoni mwangu. Nilipokutana na Yesu na kubadilishwa mwelekeo nikagundua kuwa, furaha na amani ya kweli inapatikana kwake. Sasa naishi nikiwa na matumaini makubwa ya maisha ya milele.

Endelea Kusoma Sikiliza Tazama

MESHAK SALUM HASANI

“Nilionekana kuipenda dini yangu toka utotoni. Na, hata, nilipopelekwa madrasa, nilijisomea kwa bidii na kufikia darasa la sita la Kiarabu.Toka wakati huo, niliendelea na kufuzu kama ustadhi. Kwangu, mimi, dini ilikuwa kila kitu.” Mungu katika ndoto na alinimbia, ‘Hassan, usipoacha uchawi utakufa!’ Sauti ile ilinikosesha amani. Nililazimika kwenda kwenye maombi mlimani, kwa miezi miwili mfululizo,nikimlilia Mungu. Baada ya muda,Mungu alinitahadharisha, ‘Ukitafuta kanisa, litakusaidia.’

Endelea Kusoma Sikiliza Tazama

JONAS SIMON

Moyoni mwangu, nilijua kuwa ugonjwa niliokuwa nao ulitokana na makosa niliyoyafanya, nilipochochewa na kiburi cha pesa nilizozipata nikiwa kijana. Kila nilipoomba, niliamini kuwa Mungu alinisamehe na,kama ningekufa nikiwa katika hali ile,bila shaka ningeingia mbinguni!Imani hii ilinipelekea kulia mbele za Mungu nikimsihi ili aipokee roho yangu. Maisha yangu yaliyojawa na mashaka sana.Miaka ilienda mbio na, ingawa niliendelea kudhoofu, sikuwa na wasiwasi, Mungu akaniokoa na kuniponya.

Endelea Kusoma Sikiliza Tazama

USHUHUDA WA BAHATI JOSEPH ONGONG’A

Amani, furaha na tumaini ziliyeyuka katika maisha yangu, hayo ni baada ya ajali mbaya ya gari iliyopelekea kukatwa mguu wangu wa kulia na kuniachia mateso na maonzi mengi. Lakini ashukuriwe Mungu wangu, aliyeniinua tena kutoka mavumbini, na kunirejeshea tumaini jipya lenye furaha na amani tele yanayonifanya nisonge mbele hata katika hali hii niliyo nayo. Nikutie moyo wewe unayepitia mateso pengine kama niliyopitia au zaidi, kuacha kulalamika na kuona tatizo lako kama mlina mkubwa na ugeuze macho yako sasa ukamatazame Mungu, aliye msaada wetu

Endelea Kusoma Sikiliza Tazama

ASKOFU JOHN SAID MAGENYEKA

Nilipokuwa katika njiapanda ya udini, huku moyoni nikitaabika kuhusu imani ya kweli, nilimuomna Mungu, anionyeshe njia sahihi itakayoniweka huru mbali na jehanamu ya moto inayokuja. Nikiwa katika dimbwi la mawazo Mungu kupitia ndoto akanionesha njia ya kweli, ninayoisimulia leo.

Endelea Kusoma Sikiliza Tazama

DK. JOE MZIWANDA (Kiongozi wa Dini)

Mafanikio bila Mungu sawa na kujilisha upepo. Ni kuwa na furaha bila amani ya kweli. Niliishi maisha ambayo, licha ya kuwa yenye furaha, sikupata amani ya moyo. Hii ilinipelekea kuwaza sana siku moja na, hatimaye, niliamua kuchukua maamuzi sahihi. Maamuzi yale ndiyo yaliyoniwezesha kupata amani iliyoambatana na furaha niliyoitafuta kwa muda mrefu.”

Endelea Kusoma Sikiliza Tazama

MASULU MAKASSY

“… Kupitia muziki, nilijipatia marafiki wengi sana, akiwemo Idd Amin Dadaa, kabla ya kumpindua Milton Obote na kuutwaa Urais wa Uganda. Pamoja na hayo nilipitia mambo magumu na mazito katika maisha yangu nikiwa nchini, Uganda, ikiwamo kuwekwa maabusu chumba kidogo pamoja na maiti kwa siku tatu! Baada ya kumpokea Kristo, Bwana na Mwokozi wa maisha yangu, niliamua kumtumikia Mungu kwa njia ya uimbaji.”

Endelea Kusoma Sikiliza Tazama