Hadithi zinaweza kubadilisha maisha yako

Hakuna mtu hapa duniani anayeponyoka kutoka kwa matukio ambayo yalimsababisha maumivu na unyanyasaji kutoka kwa watu tofauti ambao ni mbali au hata karibu sana na sisi. Kwa ujumla, matukio haya huacha ndani yetu makovu na vidonda moyoni mwetu ambavyo vinabaki hata na wakati unaopita. Ni ngumu zaidi wakati chuki kwa watu hawa inatuongoza kulipiza kisasi. Kisasi hiki ni hatari kwa ubinafsi wetu kwa sababu hisia hizi za kulipiza kisasi zinaweza kuathiri matendo na maamuzi yetu kwa kila mtu karibu nasi. Kwa kuongezea, kulipiza kisasi hiki kunasababisha turuba ya giza ambayo huua hisia zote za wanadamu na inaweza kuharibu uwetu wetu kama vile wakati wetu ujao na maisha yetu yote. Nguvu ya msamaha inatupa uhuru kutoka kwa chuki. Watu ambao wamepigana wakawa huru na amani katika mioyo yao na roho. Ushuhuda huu unathibitisha nguvu ya uponyaji ya Mungu, iliyo ndani ya watu kugusa kwa upendo na huruma; hii pia iliiponya mioyo yao, ilibadilisha maisha yao na ikawasamehe. Haijalishi uzoefu wako, asili yako, ngono, unaangaziwa na ugunduzi mkubwa zaidi duniani upendo wa Mungu na fanya mazoezi ya msamaha katika maisha yako mwenyewe.
Hadithi

USHUHUDA WA BAHATI JOSEPH ONGONG’A
Amani, furaha na tumaini ziliyeyuka katika maisha yangu, hayo ni baada ya ajali mbaya ya gari iliyopelekea kukatwa mguu wangu wa kulia na kuniachia mateso na maonzi mengi. Lakini ashukuriwe Mungu wangu, aliyeniinua tena kutoka mavumbini, na kunirejeshea tumaini jipya lenye furaha na amani tele yanayonifanya nisonge mbele hata katika hali hii niliyo nayo. Nikutie moyo wewe unayepitia mateso pengine kama niliyopitia au zaidi, kuacha kulalamika na kuona tatizo lako kama mlina mkubwa na ugeuze macho yako sasa ukamatazame Mungu, aliye msaada wetu

CHARLES LUOGA
Mimi nimekuwa shahidi wa matendo makuu ya Mungu. Nimelisoma na kuliishi neno lake. Nimemuona Mungu akinitendea na kuwatendea wengine.Pia, nimewaona watu mbali mbali, katika huduma yangu na kwingineko, wakiendelea kuukulia wokovu. Kupitia muujiza huu, pendo na utumishi wangu kwa Mungu vimeongezeka. Ninataka nikuhakikishie wewe, unayeusoma ushuhuda huu, kuwa Mungu yupo. Anatenda miujiza, huwalinda watu wake, na kuwaponya

COSMAS CHIDUMULE
Maisha ya starehe nyingi, nilipokuwa katika ulimwengu wa muziki duniani hayakunifanya nifikie kwenye utoshelevu wa furaha na amani ya kweli moyoni mwangu. Nilipokutana na Yesu na kubadilishwa mwelekeo nikagundua kuwa, furaha na amani ya kweli inapatikana kwake. Sasa naishi nikiwa na matumaini makubwa ya maisha ya milele.

USHUHUDA WA MUNA LOVE
“MUNGU anazo njia nyingi anazotumia kuokoa watu wake, kwa ajili ya kusudi lake mwenyewe. Alimtumia mtoto wangu akiwa na umri wa miaka sita, kugeuza mtazamo wangu wa imani, siku chache baadaye Mungu alimtwaa. Machungu ya kumpoteza yanazimwa na kauli zake zilizoungamanishwa na upendo wa Mungu ulionivuta mimi kwenye wokovu. Natatangaza fadhili za Bwana katika maisha yangu yote!

BOAZ DAVID MWASOTA
Maisha ya kutumia mihadarati na uporaji yalinitenga mbali na familia. Jamii yangu ilinichukulia kuwa kama ‘mbwa mwitu,’ aliyeishi katikati ya watu. Niliadahika nikidhani kuwa, kwa kufanya hivyo, ningeondokana na upweke. Kumbe haikuwa hivyo! Nilijiongezea matatizo yaliyochangia kujiangamiza kimaisha. Ashukuriwe Mungu aliyeniona, tokea mbali na kunivuta ili kuniingiza katika pendo lake na kuniondolea aibu, leo nathubutu kusimulia matendo yake makuu.”

JONAS SIMON
Moyoni mwangu, nilijua kuwa ugonjwa niliokuwa nao ulitokana na makosa niliyoyafanya, nilipochochewa na kiburi cha pesa nilizozipata nikiwa kijana. Kila nilipoomba, niliamini kuwa Mungu alinisamehe na,kama ningekufa nikiwa katika hali ile,bila shaka ningeingia mbinguni!Imani hii ilinipelekea kulia mbele za Mungu nikimsihi ili aipokee roho yangu. Maisha yangu yaliyojawa na mashaka sana.Miaka ilienda mbio na, ingawa niliendelea kudhoofu, sikuwa na wasiwasi, Mungu akaniokoa na kuniponya.

ASKOFU JOHN SAID MAGENYEKA
Nilipokuwa katika njiapanda ya udini, huku moyoni nikitaabika kuhusu imani ya kweli, nilimuomna Mungu, anionyeshe njia sahihi itakayoniweka huru mbali na jehanamu ya moto inayokuja. Nikiwa katika dimbwi la mawazo Mungu kupitia ndoto akanionesha njia ya kweli, ninayoisimulia leo.

AMOS HAMIS (Shoga Aliyeokoka)
“Yasiyowezekana kwa binadamu kwa Mungu yanawezekana.” hivi ndivyo ninavyoweza kukiri, ninapoaksi maisha yangu mimi, yaliyosheheni matukio mengi magum ya aibua, yaliyochefua na kusababisha nikataliwe mbali na jamii, ambayo kwa hayo akili za kibinadamu haikuwa vigumu kubadilika, sasa na weza kusema Mungu anaweza kumbadilisha mtu muovu na kumheshimisha tena katika jamii.

DK. JOE MZIWANDA (Kiongozi wa Dini)
Mafanikio bila Mungu sawa na kujilisha upepo. Ni kuwa na furaha bila amani ya kweli. Niliishi maisha ambayo, licha ya kuwa yenye furaha, sikupata amani ya moyo. Hii ilinipelekea kuwaza sana siku moja na, hatimaye, niliamua kuchukua maamuzi sahihi. Maamuzi yale ndiyo yaliyoniwezesha kupata amani iliyoambatana na furaha niliyoitafuta kwa muda mrefu.”